Mashamba makubwa ya miti kwa ajili ya viwanda yanavyovamia Mashariki na Kusini mwa Afrika

SWAHILI. Taarifa hii ya pamoja kati ya Timberwatch Coalition na World Rainforest Movement inalenga katika mambo mbalimbali ya ndani na nje yanayojulisha kuhusu hali ya mabadiliko ya mashamba makubwa ya miti kwa ajili ya viwanda katika nchi 11 za Mashariki na Kusini mwa Afrika. Kwa mashamba makubwa ya miti kwa ajili ya viwanda (ITPs), tuna maana mashamba makubwa ya miti ya aina moja yanayosimamiwa kwa umakini, yenye umri unaolingana mingi ya hiyo ni ya jamii ya mikaratusi, misindano au migunga (acacia) ambayo siyo ya asili, ambayo imepandwa kwa lengo kuu la kupata timbao kwa ajili ya mchakato wa uzalishaji viwandani, au kwa ajili ya shughuli nyingine za biashara kama vile biashara katika kaboni inayoongezeka.

Download  Mashamba makubwa ya miti kwa ajili ya viwanda yanavyovamia Mashariki na Kusini mwa Afrika